Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, aliongoza ujumbe wa Mabalozi wa SADC kufanya mazungumzo na Serikali ya Brazil yaliyowakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Kenneth Felix Haczynski da Nobrega, Secretary of Bilateral Negotiation in the Middle East, Europe and Africa, ambapo aliwasilisha “demache” ya kuiomba Serikali ya Brazil kuunga mkono jitihada ya SADC ya kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuifutia Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi.