Balozi Dkt. Nchimbi aliongoza ujumbe wa Mabalozi kumi (10) wa nchi wanachama wa SADC kuonana na Mhe. Balozi Kenneth Felix Haczynski, Naibu Waziri wa Brazil anayeshughulikia mahusiano ya Mashariki ya Kati, Ulaya na Afrika. Lengo la mazungumzo haya ilikuwa kuitambulisha Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC) nchini Brazil lakini pia kuomba ushiriki wa Brazil katika utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya Jumuiya hiyo.  Mabalozi walioshiriki mazungumzo haya ni pamoja na Balozi wa Namibia, Zambia, Malawi, Afrika Kusini, Botswana, Angola, DRC, Zimbabwe, Msumbiji na Tanzania.