Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi alifanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) chini ya Taasisi ya Centre for Excellence for Hunger ya Brazil Bw. Peter Rodrigues aliyeambatana na Bw. Gregory Rosa, Afisa mratibu wa Shirika hilo. Mazungumzo hayo yalilenga katika mradi mpya wa uzalishaji wa bidhaa zitokazanazo na zao la pamba ukiendana na kilimo mseto. Bw. Peter anatarajiwa kuitembelea Tanzania mnamo tarehe 9 hadi 16 Februari, 2019 kwa lengo la kujadiliana na wadau mbalimbali kuhusu mradi huu wa ushirikiano.