Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya kuimarisha sekta ya madini nchini, Ubalozi umefanikiwa kuratibu ziara ya mafunzo kwa ujumbe wa Serikali wa Wizara ya Madini uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Samwel Msanjila. Ziara hiyo imetoa fursa kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo Sera na Sheria zilizopo za Brazil katika uchimbaji wa madini ya Rare Minerals.
