Kufuatia mwaliko wa Serikali ya Jamaica, Balozi Dkt. Emmanuel alishiriki katika wiki ya diplomasia iliyoandaliwa na Gavana Generali Sr. Patrick Linton Allen iliyoanza mnamo tarehe 2 hadi 5 Machi, 2020. Shughuli hii iliyohudhuriwa na Mabalozi wa nchi 21 kwa lengo la kuwafahamisha mwelekeo wa Serikali ya Jamaica katika utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje na mikakati ya kuimarisha ushirikiano na nchi rafiki. Shughuli hii ilifunguliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa Mhe. Kamishna Johnson Smith mnamo tarehe 3 Machi, 2020 na mnamo tarehe 5 kuhudhuria dhifa ya Taifa iliyoandaliwa na Gavana Generali wa nchi hiyo.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Balozi Dkt. Nchimbi alitumia fursa hiyo kuonana kwa mazungumzo na Mawaziri mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na Jamaica. Mawaziri hao ni  pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Delroy Chuck; Waziri wa Utalii Mhe. Edmund Bartlett; Waziri wa Viwanda, Biashara, Kilimo na Uvuvi Mhe. Floyd Green.