Mnamo tarehe 19 na 20 Februari, 2019, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi alifanya mkutano na Jumuiya ya Watanzania kwa lengo la kuwasilikiliza changamoto walizonazo na kutafuta ufumbuzi. Balozi Dkt. Nchimbi aliwaasa Watanzania hao kuendelea kufuata sheria za nchi ya Brazil lakini pia kuunga mkono juhudi za Serikali ya kupambana na vita dhidi ya matumizi na usafirishaji wa madawa ya kulevya.