Mheshimiwa Dkt. Emmanuel J. Nchimbi, Balozi wa Tanzania nchini Brazil alimwakilisha Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Jair Bolsonaro, Rais wa Brazil, zilizofanyika Brasilia tarehe 1 Januari, 2019. 

Aidha, Mhe. Balozi Nchimbi aliwasilisha ujumbe wa salamu za pongezi kwa Rais Jair kupitia kwa Waziri Mteule wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mheshimiwa Ernesto Araujo mnamo tarehe 2 Januari, 2019 wakati wa mkutano wa Waziri huyo na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Brazil.